Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kambi ya UM ya michezo kwa vijana imeanza Doha, Qatar

Kambi ya UM ya michezo kwa vijana imeanza Doha, Qatar

Mshauri maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya michezo kwa maendeleo na amani Wilfred Lemke Jumatatu amezindua siku kumi za kambi maalumu ya uongozi kwa vijana wasiojiweza kutoka mataifa tisa ya Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara na mamlaka ya Palestina.

Kambi hiyo ambayo inafanyikia Doha Qatar ni majaribio ya kuwawezesha vijana 30 ili kuanzisha programu za michezo na kuchagiza kuleta mabadiliko katika jamii zao. Alice Kariuki na taarifa kamili.

(RIPOTI YA ALICE KARIUKI)