Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mzunguko wa machafuko jimbo la Jonglei lazima ukome:UM

Mzunguko wa machafuko jimbo la Jonglei lazima ukome:UM

Afisa wa ngazi za juu wa Umoja wa Mataifa amesema mzunguko wa machafuko baina ya makabila kwenye jimbo la Jonglei Sudan Kusini lazima usitishwe. Bi Hilde F.Johnson ambaye ni mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini humo ameitaka serikali, makanisa, makundi ya jumuiya za kijamii na jamii husika kutimiza wajibu wao wa kuhakikisha amani inapatikana katika jimbo la Jonglei.

Bi Johnson amekwenda wmishoni mwa wiki kwenye jimbo hilo ambako jamii ya Lou Nuer imekuwa ikipambana na jamii ya Murle. Maelezo zaidi na George Njogopa.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)