Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano kuhusu hali ya baadaye nchini Somalia waandaliwa Nairobi

Mkutano kuhusu hali ya baadaye nchini Somalia waandaliwa Nairobi

Waziri mkuu wa Somalia Abdiweli Mohamed Ali yuko mjini Nairobi nchini Kenya kuhudhuria kikao cha Umoja wa Mataifa ambacho kitazungumzia mzozo nchini Somalia na kuchunguza kutekelezwa kwa barabara ya amani inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa.

Barabara hiyo inatoa mwelekeo wa njia za kumaliza kipindi cha mpito nchini Somalia na hatua zinazostahili kutekelezwa kabla muda wa serikali ya mpito haujakamilika mwezi Agosti mwaka ujao. Serikali ya sasa ya mpito inatakiwa kuongoza shughuli za kutekelezwa kwa mpango huo kwa ushirikiano na bunge la mpito na pande zingine zikiwemo wanawake, jamii za wafanyibiashara, viongozi wa kidini, wazee na vijana.