Hakuna msamaha kwa wakiukaji wa haki za binadamu nchini Yemen:Pillay

6 Januari 2012

Mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navi Pillay amewashauri watoa maamuzi nchini Yemen kuheshimu sheria ya kimataifa dhidi ya utoaji msamaha kwa vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu.

Pillay amesema kuwa amekuwa akifuatilia matukio nchini Yemen hasa mjadala kuhusu sheria ya utoaji msamaha utakaowasilishwa bungeni hivi karibuni. Pillay ameongeza kuwa msamaha hauruhusiwi kama utazuia kufikishwa mahakama wale watakaohusika na ukikaji wa haki za binadamu ukiwemo uhalifu wa kivita, uhalifu dhidi ya ubinadamu na mauaji ya halaiki.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud