Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahiga ashangazwa na mzozo unaondelea kwenye bunge la Somalia

Mahiga ashangazwa na mzozo unaondelea kwenye bunge la Somalia

Mjumbe maalum wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia balozi Augustine Mahiga hii leo ameelezea kushangazwa kwake kutokana na mzozo unaoendelea kati ya wabunge nchini Somalia. Ametaka pande zote kujitenga na ghasia za aina  yoyote na kutatua shida zao kwa njia ya mazungumzo ya kisiasa na kwa njia ya sheria.

Mahiga amesema kuwa ghasia ambazo zimeshuhudiwa bungeni kwa siku chache zilizopita ni jambo la kujutia na kuongeza kuwa hatua ni lazima zichukuliwe kwa waliochochea ghasia hizo. Mahiga pia ameonyesha huruma kwa wale waliojeruhiwa na kuwatakia nafuu ya haraka.