Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mvua na mafuriko yasababisha athari kwa wakimbizi nchini DRC

Mvua na mafuriko yasababisha athari kwa wakimbizi nchini DRC

Maelfu ya wakimbizi raia wa Angola waliotorokea nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo kwa sasa wamekwama kwenye mafuriko kaskazini mashariki mwa Angola. Takriban watu 50,000, 24,000 kati yao wakiwa ni wale waliorejea kwenye vijiji kumi vya mkoa wa Uige ulio karibu na mpaka wa DRC wameathiriwa na mafuriko na mvua ya mawe kwa muda wa miezi minne iliyopita huku karibu nyumba 1,142 zimeharibiwa na mvua.

Wakimbizi hao waliokimbia mapigano nchini Angola yaliyomalizika mwaka 2002 ni changamoto kubwa kwa wenyeji. George Njogopa na taarifa kamili.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)