Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Saudi Arabia yatakiwa kuondoa hukumu ya kifo

Saudi Arabia yatakiwa kuondoa hukumu ya kifo

Utawala nchini Saudi Arabia umetakiwa kuondoa kutumika kwa hukumu ya kifo. Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa OHCHR inasema kuwa imetiwa wasiwasi na kuongezeka kwa hukumu za vifo zilizotolewa mwaka 2011.

Kulingana na mashirika ya haki za binadamu ni kwamba watu 27 walinyongwa mwaka 2010 ambapo idadi hiyo ilipanda hadi zaidi ya watu 70 mwaka uliopita. Ofisi ya haki za binadamu ya UM pia inataka kusitishwa ukataji wa mikono na miguu ya watu wanaopatikana na hatia. Rupert Colville ni msemaji wa ofisi ya haki za binadamu mjini Geneva.

(SAUTI YA RUPERT COLVILLE)