Mfanyikazi wa ICRC atekwa nyara nchini Pakistan

5 Januari 2012

Mfanyikazi wa shirika la kimataifa la msalaba mwekundu ICRC ametekwa nyara na watu waliojihami kwenye mji wa Quetta nchini Pakistan. Khalil Rasjed Dale ambaye ni raia wa uingereza alitekwa nyara alipokuwa akirejea nyumbani kutoka kazini akitumia gari lenye nembo ya ICRC na alitekwa akiwa umbali wa kilomita 200 kutoka makao ya ICRC. ICRC bado haijabainisha ni nani waliohusika na kitendo hicho na lengo lao.

ICRC inasema kuwa itaendelea na huduma zake nchini Pakistan na kutoa wito kwa watekaji nyara kumuachilia mfanyikazi wao bila masharti.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter