IOM yasambaza msaada wa chakula kwa waathiriwa wa dhoruba nchini Ufilipino

5 Januari 2012

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limesambaza misaada ya kibinadamu kwa familia zilizoathiriwa na dhoruba kwa jina Washi kusini mwa Ufilipino na kuanza mikakati ya kuimarisha maisha ya watu waliohama makwao. Msaada wa kwanza wa bidhaa za kufanyia ukarabati mahema zilisambazwa kwa familia ambazo nyumba zao hazikuhariwa kabisa kwenye mji dwa Iligan likiwa moja ya maeneo ambayo yaliathiriwa zaidi na mafuriko yaliyosababishwa na na dhoruba hiyo.

Ukiwa msaada wa Euro 700,000 kutoka kwa idara ya misaada ya kibinadamu ya tume ya Umoja wa Ulaya, IOM itatoa makao na huduma za ukarabati kwa familia 1,894 kwenye miji ya Cagayan de Oro na Iligan. Jumbe Omari Jumbe msemaji wa IOM.

(SAUTI YA JUMBE OMAR JUMBE)

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter