Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Homa ya ndege yawaua watu kadhaa nchini China na Misri

Homa ya ndege yawaua watu kadhaa nchini China na Misri

Watu wawili wameripotiwa kuaga dunia baada ya kuugua ugonjwa wa homa ya ndege nchini China na Misri. Shirika la afya duniani WHO linasema kuwa wizara ya afya nchini China ililijulisha kuhusu ugonjwa huo baada ya mwanamme mmoja kutoka mkoa wa Guangdong kuonyesha dalili za ugonjwa huo.

Hata hivyo aliaga dunia juma moja baada ya kulazwa. Nchini Misri wizara ya afya iliijulisha WHO kuhusu kisa cha mwaname moja wa umri wa miaka 42 aliyeugua ugonjwa huo baada ya kuonyesha dalili mnamo tarehe 16 mwezi uliopita na kuaga dunia tarehe 22 za mwezi huo. Kulingana na WHO homa ya ndege imewaua watu 27 nchini China na 55 nchini Misri.