Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa OCHA aenda Sudan kujadilia hali ya ukosefu wa chakula

Mkuu wa OCHA aenda Sudan kujadilia hali ya ukosefu wa chakula

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na misaada ya usamaria mwema OCHA Bi Valerie Amosi ameelekea nchini Sudan ambako anakusudia kuwa na majadiliana na maafisa wa nchi hiyo kuhusiana na hali ya usalama wa chakula.

Akiwa nchini humo Bi Amosi ameelezea namna hali ya ukosefu wa chakula inavyoyaandama maeneo kadhaa na ametaka kuchukuliwa kwa hatua za hataka ili kunusuru hali hiyo.

Ripoti zinaonyesha kuwa majimbo ya Kusin mwa Kordofan pamoja na lile la Blue Nile yanakabiliwa na mkwamo wa ukosefu wa chakula na kuna wasiwasi wa kuzuka majanga kama vile utapiamlo kwa wakazi wa eneo hilo.

Maeneo hayo yamekuwa yakiandamwa na machafuko ya kikabila yanayozuka mara kwa mara ambayo yamesababisha kuanguka kwa shughuli za kilimo.