Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Serikali ya Marekani yachangia milioni 55 kwa UNRWA

Serikali ya Marekani yachangia milioni 55 kwa UNRWA

Serikali ya Marekani imetangaza mchango wake wa dola milioni 55 kwa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina UNRWA linalotoa huduma kwenye mashariki ya kati. Fedha hizo zitafadhili afya, elimu na huduma za binadamu kwa wakimbizi milioni 5 wa kipalestina katika eneo hilo.

Dola milioni 29 zitafadhili huduma kuu za UNRWA nchini Jordan, Syria na Lebanon, eneo la ukingo wa magharibi na Gaza. Milioni zingine 24 zitafadhili huduma za dharura za UNRWA katika eneo la ukingo wa magharibi na ukanda wa Gaza huku dola milioni mbili zitatumika kuwasaidia waliohama makwao nchini Lebanon wakati wa mzozo wa mwaka 2007.