Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ugiriki na Jamhuri ya zamani ya Yugoslavia zakubali kujadiliana kutanzua mzozo

Ugiriki na Jamhuri ya zamani ya Yugoslavia zakubali kujadiliana kutanzua mzozo

Ugiriki na iliyokuwa Jamhuri ya Yugoslavia ya Macedonoia zimekubaliana kwa msingi kuanzisha mazungumzo ya awali nchini ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kufikia suluhu juu ya mzozo wa muda mrefu kuhusiana na jina rasmi la eneo hilo.

Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu Matthew Nimetz anatarajia kuongoza majadiliano ya kutanzua mzozo huo wa jina, Mjini New York.

Majadiliano hayo ambayo yatahudhuriwa na wawakilishi toka pande zote mbili yanatazamiwa kufanyika January 16, na yatadumu kwa muda wa siku mbili.

Pande hizo kwa muda mrefu zimekuwa kwenye mzozo kuhusiana na matumizi rasmi ya jina na kila upande inadai kuwa na uhalali wa kutumia jina hilo.