Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wafanyikazi wa UM waomboleza wenzao waliouawa mwaka uliopita

Wafanyikazi wa UM waomboleza wenzao waliouawa mwaka uliopita

Shirika la Umoja wa Mataifa limeonya kuwa wafanyikazi wake wamekuwa walengwa kwenye mashambulizi ya kigaidi kote duniani. Haya yamesemwa kwenye sherehe za kuwaomboleza wafanyikazi wa Umoja wa Mataifa waliouawa mwaka uliopita. Kulingana na chama cha wafanyikazi wa Umoja wa Mataifa kimesema kuwa wafanyikazi 35 waliuawa mwaka 2011 wakiwemo walinzi wanne wanaofanya kazi na Umoja wa Mataifa.

Mashambulizi mabaya kwa wafanyikazi wa Umoja wa Mataifa mwaka 2011 yalifanyika nchini Afghanistan na Nigeria nchi ambazo Umoja wa Mataifa inatoa huduma kubwa.