UM wahitaji ushirikiano na mashirika ya kimaeneo:Sangqu

4 Januari 2012

Umoja wa Mataifa unastahili kuboresha uhusiano wa mashirika mengine ya kimaeneo ili uweze kufanikiwa katika kutatua mizozo kote duniani. Hii ni kwa mujibu wa balozi wa Afrika Kusini kwenye Umoja wa Mataifa Baso Sangqu anapochukua wadhifa wa urais kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa mwezi huu wa Januari. Balozi Sangqu anasema huku majukumu ya Umoja wa Mataifa yakiwa ni kudumisha amani na usalama mashirika ya kimaeneo yana wajibu mkubwa katika matatizo ya kimaeneo.

(SAUTI YA BASO SANGQU)

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter