Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM waandaa oparesheni za kibinadamu Sudan Kusini

UM waandaa oparesheni za kibinadamu Sudan Kusini

Umoja wa Mataifa unaandaa mpango mkubwa wa dharura wa usaidizi wa kuwasaidia maelfu ya watu kurejea makwao baada ya mizozo ya kijamii kati ya jamii ya Lou Nuer na Murle kwenye jimbo la Jongelei nchini Sudan Kusini.

Tangazo hilo linajiri kufuatia kujiondoa kwa wapiganaji wa Lou Nure kutoka mji wa Pibor baada ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa na wanajeshi wa serikali kuweka vituo vya kinga. Wapiganaji hao wanaondoka baada ya mashauriano. Hata hivyo maelfu ya watu kwa sasa wanahitaji chakula, maji na makao. Donn Bobb wa Radio ya Umoja wa Mataifa amezungumza na afisa wa shirika la kuratibu masuala ya kibinadamu la Umoja wa Mataifa OCHA Lisa Grande kuhusu hali ilivyo Sudan kusini.

(SAUTI YA LISA GRANDE)

CLIP