Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP yazindua vocha za chakula mjini Kabul

WFP yazindua vocha za chakula mjini Kabul

Shirika na mpango wa chakula duniani WFP hii leo limesaini makubaliano kufadhili mradi mpya kwa ushirikiano na wizara zikiwemo za kazi, masuala ya jamii na ya walemavu nchini Afghanistan.

Mradi huo una lengo la kuwasaidia watu maskini wanaoishi mijiji kukabiliana na bei ya juu ya vyakula. WFP inatoa dola milioni tatu kwa muda wa miezi sita kwa kutoa vocha za chakula za kila mwezi kwa watu maskini mjini Kabul. Awamu ya kwanza ya kutoa vocha hizo itaanza kati kati ya mwezi huu. Monica Morara na taarifa kamili.

(SAUTI YA MONICA MORARA)