Afrika kuwa ajenda kuu kwa FAO

3 Januari 2012

Mkuu mpya wa shirika la kilimo na mazao la Umoja wa Mataifa FAO Jose Graziano da Silva amesema kupiga vita njaa barani Afrika itakuwa ajenda kuu ya shirika hilo.

Akitoa hotuba baada ya kuchukua wadhifa huo mpya da Silva amesema kuwa ataangazia zaidi suala la kuiangamiza njaa na utapiamlo kote duniani. Bwana da Silva amesema kuwa FAO itapeleka huduma zake kwenye nchi kadhaa maskini hususani zinazokabiliwa na mizozo ya muda mrefu.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter