Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM kutoa makao kwa waliothiriwa na dhoruba nchini Ufilipino

IOM kutoa makao kwa waliothiriwa na dhoruba nchini Ufilipino

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM linafanya hima ili kutoa makao kwa maelfu ya familia zilizohama makwao baada ya kutokea kwa dhoruba kali iliyoikumba Ufilipino tarehe 17 mwezi huu. Dhoruba hiyo kwa jina Washi na ambayo pia inajulikana kwa wenyeji kama Sengong ilisomba maji, udongo, takataka kwenda vijijini na miji miwili mikubwa kwenye kisiwa cha Mindanao ambapo iliharibu nyumba 13,000 na kuwalazimu watu 400,000 kuhama makwao.

Hadi sasa ni watu 1250 walioripotiwa kuuawa. Mkuu wa ujumbe wa IOM nchini Ufilipino anasema kuwa janga hilo limeewacha wengi bila kitu na mahitaji kwa sasa ni mengi.