Skip to main content

Rais wa Baraza Kuu la UM ataka kuwe na ushirikiano kwenye masuala makuu ulimwenguni

Rais wa Baraza Kuu la UM ataka kuwe na ushirikiano kwenye masuala makuu ulimwenguni

Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ametaka kuwe na ushirikiano baina ya wanachama wa Umoja wa Mataifa hasa kwenye masuala ya mabadiliko kwenye Umoja wa Mataifa , maendeleo na ustawi wa dunia.

Kwenye ujumbe wake wa kumaliza mwaka Nassir Abdulaziz Al-Nasser amepongeza jamii ya kimataifa kwa jitihada ilizofanya kukabiliana na changamoto za ulimwengu mwaka 2011 zikiwemo hali ngumu ya uchumi, maaandamano pamoja na majanga ya kiasili na yanayochangiwa na binadamu. George Njogopa na taarifa kamili.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)