Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM washangazwa na uvamizi unaondelea mjini Cairo

UM washangazwa na uvamizi unaondelea mjini Cairo

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imeelezea kushangazwa kwake na uvamizi unaoendelea mjini Cairo nchini Misri kwenye mashirika kadhaa yasiyokuwa ya kiserikali mengi yakiwa ya haki za binadamu.

Wanajeshi wa Misri walivamia ofisi kadha za mashirika yasiyokuwa ya kiserikali na kuzifunga ambapo walichukua tarakilishi na nyaraka zingine. Mkuu wa ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa eneo la mashariki ya kati na Kaskazini mwa Afrika iliyo na makao yake mjini Geneva Frej Finniche anasema kuwa uvamizi huu ndio wa kwanza kwenye historia ya Misri.

(SAUTI YA FREJ FINNICHE)