ICRC yatuma misaada ya dharura kwenye eneo la Middle Juba nchini Somalia

30 Disemba 2011

Kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu ICRC imetuma msaada wa dharura wa madawa wakati kunapoendelea kushuhudiwa mapigano kwenye eneo la Middle Juba kusini mwa Somalia hasa maeneo ya Kismayo, Afmadow na Dhobley. Zaidi ya watu 100 waliojeruhiwa wamewasili kwenye vituo vya kutoa matibabu huku ikiwa hatari kubwa kwa raia wanaosafiri kwenda kwa vituo hivyo ambapo wengi waliojeruhiwa wakiwa bado wanangojea usaidizi.

Kwa sasa ICRC inataka pande zinazopigana kuheshimu sheria za kimataifa na kuendesha oparesheni zao za kijeshi kwa uangalifu pasipo kuwadhuru wale ambao hawashiriki kwenye mapigano hayo.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter