WHO yaelezea wasiwasi wake kuhusiana na utafiti wa virusi vya H5N1

30 Disemba 2011

Shirika la afya duniani WHO limeelezea wasi wasi wake kuhusu utafiti unaofanywa na taasisi kadha kubaini mabadiliko ya hali ya hewa kwa virusi vya H5N1 likisema kuwa heunda ugonjwa huo ukaambukiza zaidi kati ya binadamu. Hata hivyo WHO inasema kwamba utafiti unaofanywa kwa njia ya uangalifu ni lazima uendelee ili kuongeza uwezekano wa kupunguza maambukizi ya virusi hivyo.

Virusi vya H5N1 ni hatari kwa afya ya binadamu huku asilimia 60 ya wanaoambukizwa wakiaga dunia. Akiongea na radio ya Umoja wa Mataifa mjini Geneva naibu katibu mkuu wa WHO Dr Keiji Fukuda aliyasema haya kuhusu msimamo wa WHO kwenye utafiti huo.

(SAUTI YA KEIJI FUKUDA)

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter