UNHCR yashutumu mauaji ya kiongozi wa wakimbizi kwenye kambi ya Dadaab

30 Disemba 2011

Mkuu wa shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR ameelezea kusikitishwa kwake kufutia kuuawa kwa kiongozi wa wakimbizi kwenye kambi ya Dadaab iliyo kaskazini mwa Kenya. Antonio Guterres mkuu wa UNHCR alitoa taarifa yake baada ya mauaji ya mwenyekiti wa kundi la usalama na amani kwenye kambi ya Hagadera iliyo sehemu ya Daadab. Mwanmamme huyo ambaye bado jina lake halijatolewa alipigwa risasi mara kadha alipokuwa akielekea kwake.

Aliaga dunia alipokuwa alkisafishwa kwenda mjini Nairobi nchini Kenya kwa matibabu. Kundi analoongoza jamaa huyo ni la wakimbizi wa Dadaab na limekuwa la manufaa katika kudumisha usalama ndani ya kambi. Daniel Dickson wa Radio ya Umoja wa Mataifa alimuuliza Vivian Tan wa UNHCR mjini Nairobi maana ya tukio hili kwa usalama kwenye kambi.

(SAUTI YA VIVIAN TAN)

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter