Hali ya usalama yadorora kwenye jimbo la Darfur:Gambari

30 Disemba 2011

Mkuu wa kikosi cha pamoja cha Umoja wa Mataifa na kile cha Muungano wa Afrika UNAMID cha kulinda amani kwenye jimbo la Darfur nchini Sudan amesema kuwa kuendelea kuwepo ukosefu wa usalama kwenye jimbo hilo kumewazuia walinda amani kufanya kazi yao.

Ibrahimu Gambari amesema kuwa uwezo wao wa kuangalia na kuchukua hatua umevuruwa siku chache zilizopita katokana na ukosefu wa usalama kwenye sehemu za Kaskazini na Kusini mwa jimbo la Darfur. Mapigano yanaendelea kwenye sehemu kadha hasa kaskazini mwa Darfur na kusambaa kwenda eneo la Kordofan Kaskazini ambapo kiongozi wa kundi la Jem Khalil Ibrahim aliuawa.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter