Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ugonjwa wa kipindupindu ulioikumba DRC sasa waelekea ukingoni

Ugonjwa wa kipindupindu ulioikumba DRC sasa waelekea ukingoni

Ugonjwa wa kipindupindu ambao ulitapakaa katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo kwa sasa unaripotiwa kuanza kutoweka lakini hata hivyo kunasalia visa vichache vya maambukizi ya ugonjwa huo.

Maafisa wa Umoja wa Mataifa wamesema kuwa wakati mamlaka za dola zikijiandaa kutangaza kumalizika kwa balaa la ugonjwa huo, lakini majimbo mawili yamearifu juu ya wale waliambukizwa na ugonjwa huo.

Mamlaka za serikali kwa kushirikiana na mashirika ya kimataifa zimefaulu pakubwa kudhibiti kasi ya maambukizi ya ugonjwa huo na sasa zinasalia katika awamu ya mwisho mwisho kutangaza juu ya kukoma kwa maambukizi hayo.

Hata hivyo kumeripotiwa kuwepo kwa maambukizi kadhaa katika majimbo mawili ambayo maafisa wa afya wanajaribu kudhibiti hali ya mambo. Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na misaada ya usamaria mwema OCHA limepiga kambi nchini humo likizidisha juhudi za kuudhibiti ugonjwa huo.