Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yaipongeza Georgia kuhusu mustakabala wa watu wasio na makwao

UNHCR yaipongeza Georgia kuhusu mustakabala wa watu wasio na makwao

Shirika la Umoja wa Mataifa linalojihusisha na wakimbizi limekaribisha hatua ya serikali ya Georgea iliyoridhia mkataba wa kimataifa wenye nia ya kuwalinda na kuwatetea mamililoni ya watu walioko mtawanyikoni ambao hawana uhalisia wa nyumbani.

Kufuatia hatua yake hiyo, Georgea sasa inakuwa nchi 71 duniani kuridhia mkataba huo ambao kwa msingi unazingatia kuwalinda watu wanaokosa makwao walioko katika nchi za kigeni.

Mkataba huo ambao ni moja ya chombo muhimu katika unga wa kimataifa, unatazamiwa kuanza kufanya kazi rasmi nchini Georgea kuanzia mwezi March mwakani.

Kulingana na taarifa iliyotolewa na UNHCR Georgea ni moja kati ya nchi zilizoweka wazi shabaya yake katika kipindi cha mwaka huu kuwa itauleta katika vitendo mkataba huo jambo ambalo linakaribisha enzi mpya kwenye eneo hilo.