UM walaani vitendo vya uvunjivu wa haki za binadamu Ivory Coast

30 Disemba 2011

Ripoti mbalimbali zimesema kuwepo kwa ongezeko kubwa la uvunjifu wa haki za binadamu nchini Ivory Coast, Umoja wa Mataifa umelaani hatua hiyo ambayo inadaiwa kufanywa na vikisi vya waasi na imetaka ikomeshwe mara moja.

Kwa mujibu wa vikosi vya kulinda amani vya Umoja nchini humo,baadhi ya askari wamejihusisha katika vitendo vya uvunjifu wa haki za binadamu ikiwemo kufanya ubakaji, kuwatesa raia na kufanya uharibifu wa mali.

Akizungumza mjini Abidjan, Mkuu wa vikosi vya Umoja wa Mataifa Kenneth Blackman amesema kuwa hata hivyo mamlaka za serikali nchini humo sasa zimeanza kuchukua hatua ya haraka ili kudhubiti maovu hayo ambayo yamekuja kufuatia machafuko yaliibuka katika wiki ya hivi karibuni

Katika machafuko hayo ambayo ni mfululizo wa matukio baada ya uchaguzi uliopita, watu kadhaa wamepoteza maisha na wengine kujeruhiwa.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter