Kuna fursa nyingi mwaka wa 2012:UNESCO

29 Disemba 2011

Shirika la elimu, sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO linasema kuwa mwaka 2012 utakuwa ni mwaka wa fursa nyingi. Shirika hilo linasema kuwa litakuwa likiangazia umuhimu wa utamaduni kama kichocheo cha maendeleo na kuulezea umuhimu wa jamii katika suala hili.

UNESCO pia inasema kuwa kusimamishwa kwa mchango wa Marekani kwa shirika hilo kufuatia hatua ya wanachama wake wa kuikubali Palastina kuwa mwanachama ni suala lililoliweka shirika hilo katika hali ngumu.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter