Mfanyikazi wa UNICEF afariki kutokana na shambulizi la kigaidi nchini Nigeria

29 Disemba 2011

Mfanyikazi mwingine wa shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF ameaga dunia kufuatia shambulizi la kujitoa mhanga lililotekelezwa kwenye makao ya Umoja wa Mataifa mjini Abuja nchini Nigeria miezi minne iliyopita.

UNICEF inasema kuwa Fred Simiyu Willis aliaga dunia alipokuwa akiendelea kupata matibabu nchini Afrika Kusini . Simiyu raia wa Kenya amelifanyia kazi shirika la UNICEF mjini Abuja tangu mwaka 2004. Kifo cha Simiyu kinafikisha idadi ya wafanyikazi wa Umoja wa Mataifa waliokufa kufuatia shambulizi hilo kuwa watu 13 na wengine 12 wasiokuwa wafanyikazi wa Umoja wa Mataifa.

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter