Wenyeji wa jimbo la Kordofan Kusini wazidi kuhangaishwa na mapigano

29 Disemba 2011

Shirika la kuratibu masuala ya kibinadamu la Umoja wa Mataifa OCHA limesema kuwa wenyeji wa jimbo la Kordofan Kusini wanaendelea kuhangaishwa na mapigano kati ya wanajeshi wa Sudan na wale wa Sudan People’s Liberation Movement – North SPLM-N.

Kufuatia ripoti za serikali za makundi yaliyojihami yanayopita maeneo ya Darfur Kusini na kuingia Sudan Kusini na Kordofan Kaskazini watoa huduma za kibinadamu wamesitisha shughuli zao hasa sehemu zilizo eneo la Nyala-Ed Daein na Bahr el Arab.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter