Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wataka mashirika ya kiraia kujiingiza zaidi kwenye ujenzi wa Libya mpya

UM wataka mashirika ya kiraia kujiingiza zaidi kwenye ujenzi wa Libya mpya

Mwanadiplomasia wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa ili kuleta mustakabal mwema hasa katika kipindi hiki cha mpito nchini Libya, ambacho kinashuhudia kuzuka kwa vita vya kikabila vyama vya kirai vinawajibika kutoa mchango mkubwa kufanikisha ujenzi wa enzi za siasa mpya nchini humo.

Ian Martin ambaye ametembelea maeneo kadhaa nchini humo, amesema kuwa kuna haja ya kuanzisha matayarisha ya kuelekea kwenye uchaguzi mkuu na kuanza kuyajumuisha kwenye mifumo halali makundi ya waasi ambayo amesisitiza kuwa yanaweza kuchafua hali ya hewa jumla ya nchi hiyo kama yataendelea kutupwa mkono.

Katika ziara yake nchini humo,Martin ambaye anaongoza timu ya Umoja wa Mataifa inayotupia macho Libya alikutana na kufanya mazungumzo na maafisa kadhaa ikiwemo viongozi wa baraza la mpito la kijeshi, na wawakilishi wa mashirika ya kiraia.

Aliwapa moyo wananchi wa Libya akisema kuwa Umoja wa Mataifa uko na utaendelea kuwa nyuma yao kwenye nyakati hizi ambazo zinaweka mahitajio ya ujenzi mpya wa taifa hilo.