FAO na Jumuiya ya ulaya kuisadia Msumbuji kwenye sekta yake ya nafaka

28 Disemba 2011

Shirika la kilimo na mazao la Umoja wa Mataifa FAO limeisaidia musumbiji kwenye matumizi ya mbegu za hali ya juu kama moja ya njia ya kuongeza mazao ya kilimo nchini humo.

Mratibu wa mipango ya FAO chini ya ufadhli wa jumuiya ya ulaya nchini Musumbiji Jose da Graca anasema kuwa katika kuongeza mazao kwenye nchi ambayo imeshuhudia mazao ya chini duniani kwanza ni suala la uzalishaji linalopewa kipaumbele. Matunda kutoka na mradi huo unaoungwa mkono na jumuiya ya ulaya yanaonekana lakini hata hivyo wakulima wadogo takriban milioni nne wanahitaji usaidizi. Kwa sasa Musumbuji inahitaji tani milioni moja ya chakula.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud