Watu 10 wauawa kwenye mapigano katika eneo la Isiolo nchini Kenya

28 Disemba 2011

Takriban watu 10 wameripotiwa kuuawa kwenye eneo lililo kaskazini mwa Kenya la Isiolo kufuatia mapigano kati ya jamii za wafugaji zinazogombania malisho ambapo pia watu 2000 wamelazimika kuhama makwao kwa muda wa siku tatu zilizopita.

Mapigano kati ya jamii ya Turkana, Somali na Borana pia yamevuruga usafiri na kuwazuia wafugaji wengine kuwapeleka ngombe wao malishoni. Pia biashara ya maziwa ya ngamia imetatizwa huku wafanyi biashara wanaosafirisha maziwa kwenda mji wa Nairobi wakishindwa kufika malishoni. Waziri wa mifugo nchini Kenya Mohammed Kuti ametaka kuzitishwa kwa mapigano hayo akiongeza kuwa walio na silaha watapokonywa.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter