Ban ashutumu matumizi ya nguvu katika kutatua tofauti nchini Guinea Bissau

28 Disemba 2011

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameshutumu matumizi ya nguvu katika utatuzi wa mizozo nchini Guinea Bissau na kutaka kuheshimiwa kwa sheria kwenye taifa hilo la Afrika Magharibi. Ripoti za vyombo vya habari zinasema kwamba kuwa kamanda wa kikosi cha wanamaji nchini humo amekamatwa kutokana na rabsha za hapo jana zilizotajwa kama mapinduzi ya kijeshi.

Kupitia taarifa kutoka kwa msemaji wake Ban ameutaka utawala nchini Guinea Bissau kuchunguza matukio yaliyotokea akiongeza kuwa anafuatia hali hiyo. Monica Graylay wa radio ya UM alizungumza na afisa wa habari kwenye ofisi ya kuweka amani ya UM nchini Guinea Bissau akitaka kujua vile hali ilivyo.

(SAUTI YA )

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter