Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kampuni ya Gucci yatoa dola milioni 1.15 kwa shirika la UNICEF

Kampuni ya Gucci yatoa dola milioni 1.15 kwa shirika la UNICEF

Kampuni ya kuuza bidhaa za kifahari ya Gucci imetangaza msaada wa dola milioni 1.15 kwa shirika ka kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF kwa mpango wake ujlikanao kama ‘shule kwa Afrika’. Mpango huo uliobuniwa mwaka 2004 una lengo la kuwahakikishia elimu mamilioni ya watoto barani Afrika hasa ukilenga zaidi watoto wasichana , mayatima na watoto wanaoishi kwenye umaskini. Alice Kariuki na taarifa kamili.

(SAUTI YA ALICE KARIUKI)

Huku ushiriano wake na UNICEF ukingia mwaka wake wa saba, kampuni ya Gucci bado inaendelea kuufadhili mpango huo kwa sababu inaamini kwamba elimu ni kama zawadi ya milele. Hadi sasa kampuni ya Gucci imechangia zaidi ya dola milioni 10 kwa shirika la UNICEF na pia ndiyo mfadhili mkubwa zaidi kwa mpango wa ‘Shule kwa Afrika’. Mwaka 2010 Gucci ilitoa dola milioni moja na hadi sasa Gucci imetoa mchango ambo umewafikia zaidi ya watoto milioni 5.5 barani Afrika na kuboresha sekta ya elimu.