Ujumbe wa UM nchini Haiti watuma risala za rambi rambi kwa familia za waliokufa baharini

28 Disemba 2011

Mkuu wa kikosi cha Umoja wa Mataifa cha kulinda amani nchini Haiti ametuma risala za rambirambi kwa rais wa nchi hiyo na kwa familia za watu 38 ambao walikufa baharini baada ya mashua walimokuwa kuzama juma lililopita mashariki mwa pwani ya Cuba.

Mariono Fernandez mjumbe maalum wa Katibu Mkuu na mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Haiti MINUSTAH ameelezea kujitolea kwa ujumbe huo katika kusaidia utawala nchini Haiti katika jitihada zake za kuboresha maisha ya wananchi wake. Kulingana na ripoti za vyombo vya habari maiti hizo 38 zilipatikana baada ya walinzi wa pwani walipoipata mashua hiyo karibu mita 100 nje ya mji wa Pointi Maisi.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter