Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF yapongeza hatua ya Mexico kutenga bajeti kuwekeza watoto

UNICEF yapongeza hatua ya Mexico kutenga bajeti kuwekeza watoto

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na watoto UNICEF limesifu na kupongeza mpango unachukuliwa na serikali ya Mexico ambayo imeanisha shabaya ya kuboresha ustawi wa watoto pamoja na kuanza kuchukua hatua mpya za kuimarisha hali ya uchumi.

Takwimu za hivi sasa zinaonyesha kuwa karibu asilimia 27 ya watoto wanaishi vijijini wakiwa katika hali ya umaskini uliotopea ukilinganisha na asilimia 8 ya wanaoishi katika maeneo ya mijini.

Watoto wengi wanaoishi katika maeneo hayo ya vijijini wanaishi maisha ya pangu pakavu wakikosa huduma muhimu za kijamii na hata kiwango cha elimu wanachopata bado ni duni mno.

Hata hivyo hivi sasa serikali imetangaza shabaya yake ya kuweka mikakati ya kukabiliana na hali ya umaskini na imesisitiza pia haja yake ya kuwainua kiustawi watoto. Imetenga tayari mafungu ya fedha kwa ajili ya kufanikisha azma yake hiyo.

Ikipongeza juhudi hizo, UNICEF imesema kuwa kuwepo kwa mipango ya aina hiyo kunafungua ukura mpya wa matumaini kwa mamia ya watoto ambao wanaishi kwenye maisha ya dhiki na shida kubwa.