Ofisi ya haki za binadamu ya UM yataka polisi waliotenda uovu nchini Haiti kufikishwa mbele ya sheria

27 Disemba 2011

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imeutaka utawala nchini Haiti kuchunguza na kuwafikisha mbele ya sheria polisi wanaokisiwa kuendesha mauaji na mateso baada ya ripoti mbili kutoka kwa Umoja wa Mataifa kudai kuwa matumuzi ya nguvu kutoka kwa polisi huenda yalisababisha vifo vya watu tisa kwenye mji wa Port-au-Prince kati ya mwezi Oktoba mwaka 2010 na Juni mwaka huu.

Ripoti hiyo inataka kufanyika uchunguzi kwa matukio sita ambapo polisi 20 walidaiwa kuhusika kwenye vifo vya raia tisa wa Haiti. Alice Kariuki anaripoti.

(SAUTI YA ALICE KARIUKI)

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter