Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM waelezea masikitiko yake kufuatia China kuendelea kuwatia korokoroni watetezi wa haki za binadamu

UM waelezea masikitiko yake kufuatia China kuendelea kuwatia korokoroni watetezi wa haki za binadamu

Umoja wa Mataifa umeelezea masikitiko yake kufuatia hatua ya mamlaka ya China kumtia korokoroni mwanaharakati wa haki za binadamu Chen Wie ambao kwa miaka mingi amekuwa mstari wa mbele kupigania usawa na haki za watu dhidi ya utawala wa China.

Umoja wa Mataifa umesema kuwa hatua ya kutupwa jela kwa mwanaharakati huyo inatoa ishara mbaya tena inavunja nguvu juhudi za kuimarisha ustawi wa haki za binadamu.

Hukumu dhidi ya mwanaharakati huyo imekuja wiki moja tu baada ya mwana sheria mmoja na mpigania haki za binadamu Gao Zhisheng kuhukumiwa kwenda gerezani kwa kifungu cha miaka 3.

Kamishna wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navi Pillay mbali na kulaani hali hiyo lakini pia amesema kuwa uhuru na haki za msingi nchini china bado zinaendelea kubanwa.