Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mexico yaongoza jitihada za kuwekeza kwa watoto

Mexico yaongoza jitihada za kuwekeza kwa watoto

Bajeti ya mwaka 2012 nchini Mexico itajumuisha masuala ya ufumbuzi ili kuboresha maisha ya watoto. Hili linajiri baada ya wito kutoka kwa shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF wa kutaka kuwepo uwekezaji kwa watoto.

Susana Sottoli mjumbe wa UNICEF nchini Mexico anasema kwamba kuna matumani ya kuwepo bajeti hiyo wakati tatizo la umaskini likiwakabili maelfu ya watoto nchini humo.