Lengo la kuwepo maji safi ya kunywa kutimizwa kabla ya mwaka 2015:UNICEF/FAO

23 Disemba 2011

Mashirika ya Umoja wa Mataifa likiwemo la kuhudumia watoto UNICEF na lile na afya duniani WHO yametoa ripoti inayoonyesha kuwa lengo la milenia la kuhakikisha kila mmoja ana maji safi ya kunywa huenda likatimizwa kabla ya muda uliowekwa wa mwaka 2005.

Ripoti hiyo inasema kwamba karibu watu milioni 1.8 kwa sasa wana maji safi ya kunywa ikilinganishwa na mwanzo wa miaka ya tisini. Hata hivyo watu maskini wanaendelea kusalia nyuma.

Ripoti hiyo inasema kuwa kati ya mwaka tisini na 2008 idadi ya watu waliokuwa na maji safi ya kunywa iliongezeka kutoka asilimia 77 hadi 87. Monica Morara ana ripori.

(SAUTI YA MONICA MORARA)

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter