Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO na ILO watoa mwongozo wa kukabiliana na tatizo la ajira ya watoto

FAO na ILO watoa mwongozo wa kukabiliana na tatizo la ajira ya watoto

Shirika la kilimo na mazao la Umoja wa Mataifa FAO na lile la kazi dunia ILO wametoa mwongozo mpya ulio na lengo la kuwasaidia watunza sera na serikali kukabilina na suala la ajira ya watoto kwenye sekta ya uvuvi.

Wataalamu wengi wanaamini kuwa ajira za watoto kwenye uvuvi ni suala lililosambaa lakini hata hivyo takwimu kuhusu ajira ya watoto hazipatikani. Ajira za watoto kwenye sekta za uvuvi, misitu, kilimo na ufugaji zinakisiwa kuchukua asilimia sitini ya watoto milioni 215 walio kwenye ajira. Kati ya shuguhli ambazo watoto hupewa kwenye sekta ya uvuvi ni pamoja na kupika, kupiga mbizi kuondoa neti zilizokwama, kuosha samaki , kusafirisha samaki na kuuza pia.