Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP yashutumu mauaji ya wafanyikazi wake nchini Somalia

WFP yashutumu mauaji ya wafanyikazi wake nchini Somalia

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limethibitisha vifo vya wafanyikazi wake wawili na mtu mwingine mmoja anayefanya kazi na shirika moja nchini Somalia. Shambulizi lililosababisha vifo hivyo lilifanywa leo asubuhi kwenye mji wa Mataban mkoa wa Hiiran kati kati mwa Somalia.

Wafanyikazi wawili wa WFP wakiwemo Muhyedin Yarrow na Mohamed Salad walipigwa risasi na kuuawa. Wafanyikazi hao walikuwa katika eneo hilo ili kuchunguza usambazaji wa chakula kwenye kambi za wakimbizi wa ndani. Inasemekekana kwamba mwenye kuwapiga risasi alijisamilisha na kukamatwa huku shughuli za WFP zikisimamishwa katika eneo hilo.