Polisi nchini DRC wavunja sherehe za kuapishwa kwa Tshisekedi

23 Disemba 2011

Polisi kwenye Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo wamewatawanya wafuasi wa kiongozi wa upinzani Etiene Tshisekeni hii leo ili kuzuia shughuli haramu ya kuapishwa kwake. Etiene Tshisekedi alipoteza baada ya kushindwa na rais Joseph Kabila kwenye uchaguzi wa Novemba 28 lakini akapinga matokeo hao.

Kulingana na kituo cha Radio cha Okapi ambacho ni mshirika wa UM ni kuwa kulisikika milio ya risasi kwenye mji mkuu Kinshasa na maeneo yanayouzunguka uwanja wa Martyr mjini humo. Kituo hicho kinasema kuwa polisi walitumia vitoa machozi kuwatawanya wafuasi wa Tshisekedi huku idadi ndogo ya watoto wakifika shuleni na bishara chache zikiwa zimefunguliwa kulinga na mwenye kushuhudia hali anavyoeleza.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter