Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF yaitaka Misri kuwalinda watoto wakati huu wa maandamano

UNICEF yaitaka Misri kuwalinda watoto wakati huu wa maandamano

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na watoto UNICEF limeitaka mamlaka ya Misri kuweka ulinzi wa kutosha kwa watoto ili kuwalinda na madhira yoyote kufuatua maandamano ya amani yanayoendelea nchini humo.

Ametaka kuanzishwa kwa uchunguzi huru kufuatia kuwepo kwa watu waliopoteza maisha na wengine wakijeruhiwa vibaya wakati wa maandamano hayo yanayoandamwa na vikosi vya kijeshi.

Kulingana na maelezo yaliyotolewa na Waziri wa Afya, watu waliopoteza maisha wamefikia 15 na wengine zaidi 800 wakijeruhiwa kufuatia makabiliano baina ya vikosi vya usalama na waandamanaji hao.

UNICEF imesema pia idadi ya vifo vya watoto imeongezeka katika siku za hivi karibuni, na hivyo kuitaka mamlaka kuchukua hatua za haraka kuzuia mwenendo huo.