Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM waendesha shabaya ya kuwasaidia waathirika wa Philippines

UM waendesha shabaya ya kuwasaidia waathirika wa Philippines

Umoja wa Mataifa unaendesha harakati za kukusanya kiasi cha dola za kimarekani milioni 28.6 kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa dhoruba la Kitropi lililowakumba wananchi walioko Kusini mwa Philipine.

Kiasi hicho cha fedha kiliombwa miezi kadhaa iliyopita lakini hadi sasa bado hakijapatikana.

Umoja wa Mataifa pamoja na mashirika mengine ya uhisani unakusudia kuendesha miradi ya uimarishwaji wa huduma za kijamii ikiwemo maji safi ya kunywa na kuoga, vyakula, na kuweka makazi ya muda kwa familia zaidi ya 471,000 ambazo zimeathiriwa na hali hiyo.

Huduma hizo zinatarajiwa ziwe zimekamilika katika kipindi cha miezi mitatu kuanzia sasa.