Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama larefusha muda wa kusalia vikosi vya kulinda amani Abyei

Baraza la Usalama larefusha muda wa kusalia vikosi vya kulinda amani Abyei

Baraza la Usalama limerefusha muda kwa vikisi vya kulinda amani katika jimbo la Abyei ambalo linagambaniwa kati ya Sudan Kusini na Sudan kwa muda wa miezi mitano zaidi na kuzitolewa mwito pande hizo zinazozozana kuweka shabaya ya pamoja ili kutanzua mkwamo huo kwa wakati muafaka.

Kikosi cha kulinda amani kwa ajili ya eneo hilo UNISFA kilichoanzishwa June nwaka huu kilitarajiwa kumaliza muda wake mwishoni mwa mwaka huu, lakini kutokana na hali ya mkwamo unayoshuhudiwa sasa kimeongezewa muda zaidi.

Kuna hali ya msuguano wa pande zote mbili hasa baada ya Sudan Kusini kujitenga rasmi na kuwa taifa hilo hali ambayo imezusha msuguano mkubwa juu ya kumiliki eneo la Abyei ambalo linautajiri wa malia asili nyingi.

Katika azimio lake, Baraza la Usalama limetaka vikosi vya serikali ya Sudan ambavyo vilitumwa huko miezi kadhaa iliyopita kujiondosha mara moja ili kuanzisha mchakato wa amani.