Serikali ya Syria lazima isitishe mauaji ya watu:UM

Serikali ya Syria lazima isitishe mauaji ya watu:UM

Serikali ya Syria lazima izingatie makubaliano iliyotiwa saini na muungano wa nchi za Kiarabu Arab League wa kukomesha mauji ya watu.

Akizungumza kwenye mkutano wa mwisho wa mwaka na waandishi wa habari Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Balozi Abdulaziz Al-Nasser amesema baraza kuu liko makini kusaidia msaada wa kimataifa kwa ajili ya mabadiliko yanayotokea katika ulimwengu wa Kiarabu.

Al-Nasser alipoulizwa swali endapo atakuwa tayari kuzuru Syria kama sehemu ya juhudi za kumaliza miezi tisa ya machafuko na ukandamizaji kwa waandamanaji amesema, hana shida yoyote kuzuru Syria na atafurahi kuzuru lakini kwanza kabisa wanachotaka kukiona ni serikali ya Syria kusitisha ghasia na mauaji kwa watu wake na pia kutimiza ahadi zake baada ya kutia saini na muungano wa

nchi za Kiarabu.

Amesema kama inavyofahamika kutakuwa na timu itakayokwenda Syria ili kuona ni jinsi gani serikali ya Syria inatilia maanani ahadi yake.