Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kiwango cha uchumi Amerika Kusini kushuka 2012

Kiwango cha uchumi Amerika Kusini kushuka 2012

Hali ya ukuaji uchumi katika eneo la Latin Amerika na Carebbean inatazamiwa kushuka mwaka ujao kutokana na hali ya mkwamo wa uchumi wa dunia inayoshuhudiwa katika masoko kadhaa.

Kulingana na ripoti moja ya Umoja wa Mataifa, hali ya uchumi itashuka kwa asilimia 3.7 katika kipindi cha mwaka ujao wa 2012 tofauti na ilivyokuwa mwaka mmoja nyuma, ambako kulishuhudiwa anguko la asilimia 3.4

Hata hivyo ripoti hiyo imesifu namna maeneo hayo yalivyofaulu kupiga hatua kwa kujitahidi kuimarisha hali ya uchumi wake.